Saturday 11 July 2015

MAMILIONI YAKAMATWA DODOMA.




Jana majira ya saa nne za usiku, iliripotiwa kuwa Kingunge Ngombale Mwiru, Parseko Kone na Mgana Msindai walikuwa wanaratibu mkakati wa Team Lowasa wa kuanzisha harakati za kumuondoa madarakani Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete. Taarifa hiyo ilieleza kuwa wajumbe wa NEC wapatao 200 kwa nyakati tofauti walikuwa maeneo ya St Gasper ambako walikuwa wanakabidhiwa fedha na kwamba kila mjumbe alipata shilingi milioni tano za awali na kwamba kama wangefanikisha mpango huo wangepata shilingi milioni tano nyingine kwa kila mjumbe.

Mtakumbuka pia kuwa St Gasper pamoja na Nam Hotel ni hoteli ambazo zimehodhiwa na Team Lowasa na ndipo wanapopanga na kuratibu mikakati yao ovu ikiwa ni pamoja na kuhonga wajumbe wa NEC na Mkutano Mkuu. Kwa bahati mbaya sana, taarifa hiyo iliondolewa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii ikiwemo jamiiforums kwa sababu zisizofahamika. 

Katika hatua nyingine, leo majira ya saa tano hivi imeripotiwa kuwa mburushi mmoja amekamatwa St Gasper akiwa na maburungutu ya fedha. Baada ya kuhojiwa mburushi huyo, kwa maelekezo ya Hussein Bashe amesikika akisema kuwa fedha hizo ni za Benard Membe. Kwa watu ambao tunajua mkakati wa akina Kingunge hatukupata shida kubaini kuwa hizo ni njama za Team Lowasa kutaka kujinasua na kashfa za kuhonga wajumbe na badala yake ionekane kuwa ni Benard Membe.
Maelezo ya awali yaliyochukuliwa kwa mburushi huyo yanaonesha kuwa ni mfanyakazi wa kampuni ya Quality Group ya Yusuf Manji. Pia wakati anakamatwa, alikuwa pamoja na Hussein Bashe, Fadhili Ngajiro, Ole Porokwa, Omar Ng'wanang'wala ambao wote wapo Team Lowasa. Porokwa ni Katibu wa CCM wilaya ya Manyara ambaye pia ni msaidizi wa Edward Lowasa. Haihitaji darubini kung'amua kuwa ni Team Mafisadi ndio wanaocheza move hii.

Wadau, hakika Mafisadi wamenasa. Hawana pa kutokea. Wametaitiwa kila kona. Wanabaki wanatweta. Hapo St Gaster kuna maburungutu mengi ya fedha pamoja na pale Nam HOTEL ambayo yamehifadhiwa kwa ajili ya kuvuruga mchakato wa CCM kumpata mgombea Urais. Polisi pamoja na TAKUKURU wakifanya kazi ipasavyo watabaini madudu mengi sana yanayofanywa na Team Mafisadi.

No comments:

Post a Comment