Wednesday 8 July 2015

UCHUMI, TANZANIA.

BENKI ya NMB imezindua huduma inayoruhusu kutumia intaneti katika kupata huduma mbalimbali zinazohusu miamala ya fedha pamoja na kupata taarifa mbalimbali kutoka benki hiyo.
Akizungumzia huduma hiyo, jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano wa NBM, Alluthe Nungu alisema huduma hiyo ya NMB App, inatoa fursa kwa watumiaji wa intaneti kupata huduma zaidi zinazohusiana na Benki hiyo kwa kutumia simu za mkononi zenye intaneti .
“Kupitia mfumo wa NMB App wateja wataweza kuangalia salio katika akaunti zao, kutoa ama kutuma fedha pamoja na kuweza kulipia huduma mbalimbali kama kulipia kodi katika mamlaka ya mapato nchini na hata huduma za DSTv,” alisema Nungu.
Alisema ili kujiandikisha katika mfumo huo na kuweza kupata huduma, mteja atatakiwa kuwa amejisajili katika mfumo wa NMB mobile lakini ilikupata taarifa mbalimbali za kibenki mteja atawezakujisajili na kupata huduma.
Nungu alisema NMB App inatoa huduma nyingi kwa wateja wa benki hiyo ambapo hata kwa wateja ambao watakuwa nje ya nchi wataweza kupata huduma mbalimbali za kibenki kwa wakati na kwa haraka.
Alisema kupitia mfumo huo pia, mteja ataweza kuuliza ni tawi gani la benki alilo nalo karibi, na hata sehemu ambazo zinaweza kupatikana kwa ATM Mashine zinazoweza kumsaidia kupata huduma ya kibenki kwa wakati.

No comments:

Post a Comment