Wednesday 22 July 2015

JAMES LEMBELI ATANGAZA RASMI KUJIUNGA CHADEMA

Aliyekuwa Mbunge wa KahamaJamse Lembeli (CCM) ameongea na waandishi wa habari na kutanga kuhama chama cha CCM na kujiunga na CHADEMA na huku akitangaza nia kugombea Jimbo la kahama mjini huku akiwataka wanakahama wamuunge mkono kugombea jimbo hilo.
Akielezea nia yake ya kujiunga na CHADEMA ni kuona chama hiko kina mienendo mizuri na hakijihusishi na rushwa kama ilivyokuwa katika chama cha CCM. Huku akieleza kuwa katika Bunge la katiba yeye ndio alikua mbunge wa kwanza wa CCM kupiga kura ya wazi huku akiunga mkono katiba pendekezo ya Jaji Warioba.

No comments:

Post a Comment