Friday, 6 May 2016

HABARI: TANZANIA.



BALOZI mteule, Dk Asha-Rose Migiro ameapishwa na Rais John Magufuli kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na ameahidi utumishi uliotukuka utakaoendelea kuziunganisha nchi hizo mbili.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu, Gerson Msigwa mjini Dodoma jana ilieleza kuwa hafla ya kuapishwa kwa Dk Migiro ilifanyika jana katika Ikulu ndogo ya Chamwino, Dodoma na ilihudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Dk Migiro aliteuliwa na Rais kuchukua nafasi ya Balozi Peter Kallaghe aliyerudishwa nyumbani. Akizungumza baada ya kuapishwa, Dk Migiro alisema atahakikisha uhusiano na ushirikiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Uingereza unaimarishwa zaidi. Alitaja eneo mahususi la ushirikiano kuwa ni katika kuvutia uwekezaji, biashara na utalii baina ya nchi hizo mbili.

No comments:

Post a Comment